SHIRIKISHO la Soka barani Ulaya-UEFA, limezifungia klabu zote kutoka jimbo lilijitenga la Crimea kushiriki mashindano nchini Urusi. Vilabu viwili vilijiondoa ushiriki wao katika Ligi Kuu ya nchini Ukraine na kujiunga na ligi daraja la tatu nchini Urusi msimu huu na kucheza Kombe la Urusi. Rais wa Shirikisho la Soka la Ukraine, Anatoly Konkov alituma barua ya malalamiko kwa Shirikisho la Soka la Dunia-FIFA na UEFA akitaka adhabu kwa Umoja wa Soka wa Urusi. Katibu mkuu wa UEFA Gianni Infantino amesema Crimea utafanywa kuwa ukanda maalumu kukusiana na masuala ya soka. Hatua imechukuliwa kutokana na ukweli kwamba Crimea haitambuliki kimataifa na FIFA na UEFA huwa inazionya klabu kuhama mashirikisho bila kupitia taratibu husika.

No comments:
Post a Comment