Friday, December 5, 2014

WALCOTT BADO MAJERUHI.

KLABU ya Arsenal itajitupa tena uwanjani kesho kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stoke City bila ya winga wake Theo Walcott ambaye bado anauguza majeraha ya msuli. Walcott ambaye alirejea tena uwanjani na kucheza mechi mbili akitokea benchi Novemba mwaka huu naada ya kujiuguza kwa karibu mwaka mzima majeraha ya goti, aliumia msuli wakati akiwa katika majukumu ya kimataifa. Akizungumza na wana habari Wenger amesema Walcott alichomwa sindano leo hivyo hatakuwepo katika mchezo kesho na kuendelea kudai kuwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Galatasaray nao unaweza kuwa mapema sana kwake. Beki wa kushoto Nacho Monreal pia atakosa mchezo huo baada ya kuumia katika mchezo dhidi ya Southampton katikati ya wiki lakini golikipa Wojciech Szczesny yeye atakuwepo baada ya kuanza mazoezi. Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwa Arsenal kwani toka Stoke wamepanda daraja mwaka 2008, washika bunduki hao wamefanikiwa kuwafunga mara moja pekee nyumbani kwao.

No comments:

Post a Comment