MENEJA wa klabu ya Real Madrid, Carlo Ancelotti amesema hana nia ya kuongeza wachezaji katika kikosi chake wakati wa kipindi cha usajili wa dirisha dogo Januari mwakani. Madrid wamekuwa wakihusishwa na tetesi za kumtaka chipukizi wa klabu ya Cruzeiro ya Brazil, Lucas Silva ambaye alikiri mapema wiki hii kuwa anategemea kujiunga na mabingwa hao wa Ulaya katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo. Hata hivyo akiulizwa kuhusu suala la kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 na wanahabari leo, Ancelotti alijibu kuwa anafurahia kikosi alichokuwa nacho. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa kwa jinsi anavyokiona kikosi chake hadhani kama ana sababu ya kuongeza wachezaji wengine kipindi cha Januari.

No comments:
Post a Comment