Monday, December 22, 2014

SARE DHIDI YA ARSENAL YAMPA JEURI RODGERS.

MENEJA wa klabu ya Liverpool, Brendan Rodgers anadhani wachezaji wake wameonyesha uwezo wa kupambania nafasi nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu baada ya kutoa sare ya mabao 2-2 na Arsenal jana. Katika mchezo huo uliochezwa Anfield wenyeji Liverpool ndio walioanza kupata bao la kuongoza kupitia kupitia kwa Philippe Courtinho lakini bao hilo lilisawazishwa muda mchache kabla ya mapumziko na Mathieu Debuchy na kufanya timu hizo kwenda mapumziko zikitoshana nguvu. Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku wageni Arsenal wakishambulia kwa nguvu la wapinzani wao na dakika ya 64 juhudi zao hizo zilizaa matunda baada ya Olivier Giroud kufunga bao la pili ambalo nalo lilisawazishwa na Martin Skrtel katika dakika za majeruhi. Pamoja na kutofautiana na vinara Chelsea kwa alama 17 huku wakiwa kwa nyuma kwa alama nne kufikia nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi, Rodgers anaamini kuwa wanaweza kumaliza msimu wakiwa katika nafasi ya pili kama msimu uliopita. Naye Arsenal Wenger ambaye kikosi chake kiliraruriwa kwa mabao 5-1 msimu uliopita na Liverpool, amesema wachezaji wake walikuwa wakisumbuliwa na kumbukumbu hiyo mbaya. Wenger pamoja na kuwapongeza wachezaji wake kwa mchezo mzuri lakini amesema kikubwa kilichosababisha wengine wasicheze katika kiwango cha juu ni kumbukumbu mbaya walionayo kutokana na mchezo uliopita.

No comments:

Post a Comment