MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amedai kuwa hakuna mchezaji yeyote katika Ligi Kuu aliyezoea mazingira haraka kuliko Alexis Sanchez. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Chile ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea Barcelona Julai amefunga bao lake la tisa kwa msimu huu jana wakati rsenal ikiibuka na ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Southampton. Wenger amesema ni vigumu kutafuta mfano wa mchezaji aliyezoea haraka mazingira kama ilivyo kwa Sanchez kwani amekuwa na uchu wa ushindi. Sanchez sasa anakuwa amefunga mabao 14 katika mechi 22 za mashindano yote alizoichezea Arsenal toka ajiunge nao akitokea Camp Nou kwa kitita cha paundi milioni 35. Akiwa Barcelona Sanchez aliifungia mabao 47 katika mechi 141 huku akiifungia nchi yake mabao mawili katika michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika Brazil majira ya kiangazi.

No comments:
Post a Comment