WENYEJI wa michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon Guinea ya Ikweta wanajipanga kumuajiri kocha Estaban Becker kuja kuchukua ya nafasi ya Andoni Goikoetxea. Chama cha Soka cha nchi hiyo kimeamua kutomuongeza mkataba kocha huyo uliomalizika Desemba 31 mwaka jana. Rais wa chama hicho Andres Jorge Mbomio amedai kuwa wameamua kutomuongeza mkataba kocha huyo baada ya kukiuka masharti ya mkataba wa kwanza kwa kushindwa kusafiri na kikosi cha timu kwenda Ureno Desemba 16. Nchi hiyo ina wiki mbili kuandaa kikosi chao kabla ya kuanza kwa michuano hiyo ambapo wao watafungua dimba na Congo Brazzaville Januari 17 mwaka huu.

No comments:
Post a Comment