TETESI za usajili zinaoendelea kupamba vichwa vya habari ulimwenguni kwa leo ni klabu ya Real Madrid kutaka kumuongeza mkataba winga wake mahiri Gareth Bale. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na gazeti la Daily Star, Bale anatarajiwa kuongezwa mkataba ambao utamuweka Santiago Bernabeu mpaka mwaka 2021. Baada ya kutangaza kuondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu Steven Gerard mwenye umri wa miaka 34 sasa amekuwa akiwindwa na vilabu mbalimbali mojawapo ikiwa ni Los Angeles Galaxy ya Marekani ambayo imepanga kumtengea kitita cha paundi milioni 20. Klabu hiyo imepanga kumlipa Gerrard mshahara wa paundi 100,000 kwa wiki huku wakimpatia mkataba wa miaka minne kuitumikia timu hiyo. Beki mahiri wa klabu ya Borussia Dortmund Mats Hummels yuko tayari kuondoka katika timu hiyo lakini bado hajaamua kama anataka kwenda Manchester United au Arsenal. Endapo kama klabu hizo zitamuhitaji zitalazimika kutoa kitita cha cha kufikia euro milioni 50 kwa ajili ya saini ya beki huyo ambaye amekuwa na msimu usioridhisha Dortmund. Kocha wa zamani wa Manchester United David Moyes amepania kuwasajili Mohamed Salah na Arouna Kone katika klabu yake ya Real Sociedad katika kipindi hiki cha usajili. Moyes amepanga kuwachukua wachezaji wote hao wawili kwa mkopo ikiwa ni sehemu ya kuimarisha kikosi chake ili kiepuke hatari ya kushuka daraja.

No comments:
Post a Comment