Monday, January 5, 2015

AFCON 2015: ATSU AJUIMUISHWA KATIKA KIKOSI CHA GHANA

KIUNGO mahiri wa klabu ya Everton, Christian Atsu amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 26 wa timu ya taifa ya Ghana kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon inayotarajiwa kuanza baadae mwezi huu. Atsu mwenye umri wa miaka 22 alipata majeruhi ya msuli wa paja katika mchezo wa Europa League ambao Everton ilifungwa bao 1-0 nyumbani na Kuban Krasnodar Desemba 11 mwaka jana. Nyota huyo alikuwa akitegemewa kurejea katika mazoezi ya kikosi cha kwanzaJanuari 10 mwaka huu. Hata hivyo hali ilikuwa tofauti kwani Atsu ameonekana kupona haraka baada ya kutajwa katika kikosi cha Everton Alhamisi iliyopita. Mbali na hiyo kiungo huyo pia alikuwa sehemu ya kikosi cha Ghana kilichofanya mazoezi jana jijini Accra hivyo kulishawishi benchi la ufundi kumjumuisha katika safari ya kwenda Hispania. Ghana inatarajia kutangaza kikosi chake cha mwisho cha wachezaji 23 Januari 14 mwaka huu kabla ya kufunga safari kuelekea Guinea ya Ikweta kwa ajili ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment