GOLIKIPA wa kimataifa wa Brazil na klabu ya Fiorentina Neto anatarajia kuikacha timu hiyo mwezi huu au mwishoni mwa msimu baada ya kukataa kusaini mkataba mpya Jumamosi iliyopita. Katika taarifa yake klabu hiyo ilithibitisha kuwa golikipa huyo hana mpango wa kusaini mkataba mwingine na anaweza kuondoka. Neto mwenyewe amefafanua kuwa uamuzi huo hauhusiani na masuala ya fedha kwani madhumuni yake makubwa ni kutafuta changamoto nyingine. Taarifa za vyombo vya habari zimedai kuwa mabingwa wa Serie A Juventus wanamuwinda golikipa huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye alikuwepo katika kikosi cha Brazil kilichonyakuwa medali ya fedha katika michuano ya olimpiki mwaka 2012 jijini London.

No comments:
Post a Comment