Friday, January 16, 2015

MOURINHO ATAJWA KUWA KOCHA BORA WA KARNE NYUMBANI KWAO URENO.

JOSE Mourinho ametajwa kuwa kocha bora wa karne katika sherehe za miaka 100 za Shirikisho la Soka la Ureno zilizofanyika jijini Lisbon. Mourinho alipewa heshima hiyo katika sherehe hizo juzi kutokana na mafanikio aliyopata kwa kushinda mataji saba ya ligi katika nchi nne tofauti na taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Porto na baadae Inter Milan. Akihojiwa Mourinho mwenye umri wa miaka 51 amesema mataji aliyoshinda wakati akiwa na Porto ndio yalikuwa muhimu katika maisha yake ya ukocha kwasababu alishinda kwasababu ya timu ya Ureno na soka la Ureno. Mourinho aliongeza kuwa kushinda taji la Ligi ya Mabingwa akiwa na Porto nalo lilikuwa jambo la kipekee kwake kwani alishinda akiwa na wachezaji tisa wa Ureno. Katika sherehe hizo Cristiano Ronaldo ndiye aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora wa karne.

No comments:

Post a Comment