MENEJA wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amekiri makosa yanayofanywa katika safu yake ya ulinzi yanampa wasiwasi baada ya timu hiyo kung’olewa katika Kombe la Mfalme na mahasimu wao wa jiji Atletico Madrid. Kocha huyo ameonyeshwa kufurahishwa na jinsi kikosi chake kilivyoshambulia katika mchezo huo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 lakini alishindwa kuielewa safu yake ya ulinzi kw akufanya makosa ambayo yaliwapa nafasi mahasimu wao kuwaadhibu. Ancelotti amesema walipata mfumo wa kuwafunga Atletico msimu uliopita lakini sio mwaka huu kwani imekuwa timu imara. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa wamefanya makosa ambayo huwa hawayafanyi haswa katika kuondoa hatari zinazokuwepo katika lango lao na hakudhani kama wanaweza kufanya makosa kama hayo.

No comments:
Post a Comment