Friday, January 16, 2015

CAZORLA AWAONYA WENZAKE JUU YA MAN CITY.

KIUNGO mahiri wa Arsenal, Santi Cazorla amesema timu hiyo inapaswa kuwa bora kama watataka kuifunga Manchester City mwishoni mwa wiki hii. Arsenal imepoteza mchezo mmoja katika michezo yao sita ya Ligi Kuu iliyopita waliyocheza ambapo walifungwa na timu pekee ambayo iko juu yao katika msimamo wa ligi ya Southampton. Kikosi cha Arsenal kinachonolewa na Arsene Wenger kiko nyuma ya City kwa tofauti ya alama 11 kuelekea mchezo wao wa Jumapili katika Uwanja wa Etihad na ushindi utawafanya kuweka hai matumaini yao ya kumaliza katika nafasi nne za juu. Hata hivyo Arsenal wanajua hatari waliyonayo kwa City katika mchezo huo kwani msimu uliopita walilambwa mabao 6-3 katika uwanja huohuo na Cazorla anajua bila kucheza katika kiwango cha juu hawatakuwa na nafasi ya kutamba katika mchezo huo. Akihojiwa Cazorla amesema utakuwa mchezo mkubwa na kama wanataka kushinda hawana budi kuwa katika kingo chao cha juu kwasababu wanacheza na timu kubwa.

No comments:

Post a Comment