MENEJA wa klabu ya Crystal Palace Alan Pardew anatumaini Yaya Sanogo aliyemchukua kutoka Arsenal kwa mkopo ataweza kuimarika kama mchezaji katika kipindi atakachokuwa hapo. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alikamilisha uhamisho wake muda kwenda Palace Jumanne iliyopita ili aweze kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kulinganisha na ilivyokuwa Arsenal. Sanogo mwenye umri wa miaka 21 ni usajili wa kwanza wa Pardew toka kocha huyo wa zamani wa Newcastle United ateuliwe kuchukua mikoba ya Neil Warnock aliyetimuliwa kutokana na matokeo mabaya. Pardew amesema Sanogo ni mchezaji anayehitaji nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza jambo ambalo alikuwa halipati Arsenal hivyo ni matumaini yake ataisaidia klabu yake kuepuka hatari ya kushuka daraja.

No comments:
Post a Comment