MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amewaomba radhi mashabiki wa timu hiyo baada ya kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Mfalme na mahasimu wao wa jiji Atletico Madrid jana. Mapema kabla ya mchezo kuanza Ronaldo aliingia katika Uwanja wa Santiago Bernabeu akiwa amebeba tuzo yake ya Ballon d’Or kuwaonyesha mashabiki ambayo alishinda kwa mara ya pili mfululizo Jumatatu iliyopita huko Zurich, Uswiss. Lakini mambo yalikuwa tofauti uwanjani kwani Madrid walishindwa kabisa kugeuza matokeo ya mabao 2-0 waliyofungwa katika mchezo wa mkondo wa kwanza kwa michuano hiyo na kujikuta wakitoka sare ya mabao 2-2 hivyo kuondolewa kwa jumla ya mabao 4-2. Akihojiwa nyota huyo wa kimataifa wa Ureno amesema ni vigumu kuwa fiti kwa asilimia 100 katika kila mchezo. Ronaldo aliendelea kudai kuwa yeye ni binadamu wa kawaida na hatoki sayari nyingine hivyo kwa niaba ya wachezaji wenzake anaomba radhi pengine ingwezekana kufanya mambo vizuri zaidi. Madrid wanakabiliwa na mchezo mwingine wa La Liga Jumapili hii wakati watakapoivaa Getafe ili kujaribu kulinda tofauti yao ya alama moja wlaioyokuw anayo dhidi ya mahasimu wao Barcelona.

No comments:
Post a Comment