MENEJA wa klabu ya Juventus, Massimiliano Allegri amesisitiza kuwa hawana mpango wa kumuuza Sebastian Giovinco katika kipindi cha karibuni. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akihaha kupata namba katika kikosi cha kwanza msimu huu huku taarifa zikidai kuwa Juventus wako tayari kupekea fedha kwa ajili ya kumuuza nyota huyo wa kimataifa wa Italia. Hata hivyo, Giovinco alianzishwa katika mchezo wa jana dhidi ya Verona na kufunga mabao mawili ambayo yaliisaidia Juventus kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-1. Akihojiwa mara baada ya mchezo huo Allegri amesema Giovinco hayuko sokoni na pamoja na kuwepo mazungumzo mengi yeye mwenyewe hajaonyesha nia yeyote ya kuondoka.

No comments:
Post a Comment