BINGWA mara tatu wa masumbwi ya uzito wa juu duniani Muhammad Ali amerejeshwa tena hospitali kwa matibabu baada ya kupata maambukizi katika njia ya mkojo. Msemaji wa familia Bob Gunnell amesema Ali mwenye umri wa miaka 72 yuko katika hali nzuri na alikuwa akitarajiwa kuruhusiwa muda wowote hivi leo. Ali aliruhusiwa kutoka hospitali mapema mwezi huu kufuatia kulazwa kwa muda wa wiki mbili. Bondia huyo Mmarekani alistaafu rasmi masumbwi mwaka 1981 kabla ya kugundulika kuwa ugonjwa wa kutetemeka viungo au Parkinson mwaka 1984.

No comments:
Post a Comment