Friday, January 16, 2015

WENGER ADAI TUZO ZA BALLON D'OR HAZINA MPANGO.

MENEJA wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amesema haungi mkono kabisa tuzo za ballon d’Or na kusisitiza kuwa hakubali nafasi yeyote atakayopewa kuchagua mchezaji bora wa dunia. Cristiano Ronaldo alishinda tuzo hiyo kwa mara ya tatu Jumatatu iliyopita baada ya kufunga jumla ya mabao 61 kwa klabu na nchi yake mwaka 2014 wakati Real Madrid ikishinda taji lake la 10 la Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe la Mfalme. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ambaye aliweka rekodi kwa kufunga mabao 17 katika michuano ya Ligi ya Mabingwa alipata mara mbili zaidi ya kura alizopata Lionel Messi wakati golikipa wa Bayern Munich Manuel Neuer yeye akikaribiana na nyota huyo wa Barcelona. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo Wenger amesema haungi mkono tuzo hizo na hatakuja kumpigia kura yeyote kwasababu hakubaliani na suala hilo.

No comments:

Post a Comment