MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Ufaransa, David Ginola ametangaza kupambana na Sepp Blatter katika kinyang’anyiro cha urais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Ingawa ametangaza hivyo lakini hakuna uhakika kama Ginola ataendelea na nia yake kwani atahitaji kuungwa mkono na vyama vitano vya soka na kigezo kingine anapaswa kuwa amejihusisha na soka kwa miaka miwili kati ya mitano iliyopita. Ginola mwenye miaka 47, alikuwa kiitumikia klabu ya Paris Saint-Germain kabla ya kujiunga na Newcastle United kwa kitita cha paundi milioni 2.5 mwaka 1995. Zoezi la uteuzi wa nafasi ya urais wa FIFA litafungwa Januari 29 mwaka huu. Makamu wa rais wa FIFA Prince Ali Bin Al Hussein na mjumbe wa zamani Jerome Champagne ambaye alijiunga na FIFA mwaka 1999 ndio wagombea wengine waliotangaza nia ya kugombea nafasi hiyo. Blatter ambaye amekuwa akiiongoza FIFA toka mwaka 1998 atakuwa akigombea kwa kipindi cha tano katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Mei mwaka huu.

No comments:
Post a Comment