Thursday, January 15, 2015

TETESI ZA USAJILI ULAYA: CITY WAMTENGEA MESSI PAUNDI MILIONI 480, ARSENAL YAWATENGEA GUNDOGAN NA HUMMELS PAUNDI MILIONI 63.

KATIKA tetesi za usajili zilizopamba vichwa mbalimbali vya habari katika mitandao na magazeti barani leo ni pamoja na meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini ameripotiwa kumtengea kitita cha paundi milioni 480 mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi. Kwa upande mwingine Arsenal nao wameanza mazungumzo na klabu ya Borussia Dortmund juu ya dili la paundi milioni 63 kwa ajili ya kumsajili kiungo Ilkay Gundogan na beki wa kati Mats Hummels. Klabu za Paris Saint-Germain, Porto na Juventus zote zimeripotiwa kumuwinda winga wa Manchester United Adnan Januzaj mwenye umri wa miaka 19. Crystal Palace wao wanakaribia kufikia kiwango cha paundi milioni nane kiliwekwa na Swansea City kwa ajili ya kusajili mshambuliaji Bafetimbi Gomis mwenye umri wa miaka 19 huku kwa upande wa West Bromwich Albion wao wakimtolea macho kiungo wa United Darren Fletcher. Swansea wao wana matumaini ya kutumia fedha walizopata katika mauzo ya Wilfried Bony aliyekwenda Manchester City kwa kutenga kitita cha paundi milioni tano kwa ajili ya kiungo wa Stuttgart Alexandru Maxim mwenye umri wa miaka 24. United wameanza mazungumzo na klabu ya PSG juu ya uwezekano wa kumsajili beki wa kimataifa wa Brazil Marquinhos mwenye umri wa miaka 20 kwa kitita cha paundi milioni 30. Meneja wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho anatarajiwa kuwaachia mawinga wake Andre Schurrle mwenye umri wa miaka 24 na Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 22 kwa matumaini ya kutumia fedha hizo kwa ajili ya kumuwania beki wa Real Madrid Raphael Varane mwenye umri wa miaka 22.

No comments:

Post a Comment