Thursday, January 15, 2015

ZAMPARINI AISHUSHUA MAN UNITED.

RAIS wa klabu ya Palermo, Maurizio Zamparini amedai kuwa klabu ya Manchester United na nyingine hazitaweza kumchukua mshambuliaji Paulo Dybala katika kipindi hiki lakini anaweza kumuuuza nyota huyo wa Argentina mwishoni mwa msimu huu. Dybala mwenye umri wa miaka 21 ambaye bado hajaitumikia timu ya taifa ya wakubwa ya Argentina anaweza pia kuzitumikia Italia na Poland. Nyota huyo amefunga mabao tisa katika Serie A msimu huu na amekuwa kiatajwa kama Sergio Aguero mpya toka ajiunge na klabu hiyo akitokea Cordoba mwaka 2012. Zamparini amesema mcheza huyo ana thamani ya zaidi ya euro milioni 40 lakini hawezi kumuuza kabla ya mwezi Juni. Rais huyo aliendelea kudai kuwa vilabu vingi vimeonyesha nia ya kumtaka chipukizi huyo mojawapo wakiwa United lakini tayari ameshawaambia kuwa nyota huyo hauzwi kwasasa lakini wanaweza kuzungumza tena baada ya miezi sita.

No comments:

Post a Comment