KLABU za Tottenham Hotspurs, Bradford na Southampton jana zilifanikiwa kutinga hatua ya ya mzunguko wa nne wa michuano ya Kombe la FA baada ya kushinda michezo yao ya mzunguko wa tatu. Spurs wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa White Hart Lane, waliipiga Burnley kwa mabao 4-2 ambapo sasa watakwaana na Leicester City katika uwanja huohuo Januari 24 mwaka huu. Southampton wao wakicheza ugenini, walifanikiwa kuichapa Ipswich Town kwa bao 1-0 ambao lilifungwa na Shane Long, dakika ya 19 ya mchezo. Kwa upande wa Bradford wao walifanikiwa kupata ushindi mnono kwa kuibugiza mabao 4-0 Millwal. Michezo ya raundi ya nne itaanza kupigwa Januari 23.

No comments:
Post a Comment