Thursday, January 15, 2015

NILIKUWA SINA RAHA BAYERN - SHAQIRI.

MCHEZAJI mpya wa klabu ya Inter Milan, Xherdan Shaqiri amebainisha kuwa alikuwa hana furaha akiwa Bayern Munich kutokana na kukosa namba katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. Hata hivyo Shaqiri amekiri katika kipindi chaote alichokuwa na mabingwa hao wa Bundesliga kumemfanya aimarike kama mchezaji. Nyota huyo wa kimataifa wa Switzerland mwenye umri wa miaka 23 alijiunga na Bayern akitokea FC Basel mwaka 2012 na alionyesha kung’aa katika msimu wa kwanza lakini baadae alionekana kupwaya na kushindwa kumshawishi Pep Guardiola kumuweka katika kikosi cha kwanza. Aklihojiwa Shaqiri amesema hakuwa na furaha moja kwa moja akiwa na Bayern kwani alikuwa akikosa nafasi ya kucheza na hiyo ndio njia pekee ya kuonyesha thamani yake. Hata hivyo Shaqiri aliendelea kudai kuwa amejifunza mambo mengi alipokuwa Bayern na kucheza na wachezaji wengi wakubwa hivyo atajaribu kutumia uzoefu wake kujaribu kushinda mataji Inter.

No comments:

Post a Comment