Thursday, January 15, 2015

WANYAMA KUKAA NJE WIKI TANO.

MENEJA wa klabu ya Southampton Ronaldo Koeman anahofu Victor Wanyama anaweza kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha zaidi ya wiki tano baada ya kiungo huyo kupata majeruhi ya msuli wa paja katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Ipswich Town uliochezwa jana. Wanyama alitolewa nje dakika chache kabla ya mapumziko katika mchezo huo wa marudiano ambao Southampton alishinda bao 1-0. Koeman amesema kutokana na ratiba ilivyo alikuwa amepanga kumchezesha Wanyama kwa dakika 45 ili kumpa muda wa kumpumzika kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu lakini hali imekuwa tofauti. Wanyama amekuwa sehemu muhimu katika kikosi cha Koeman msimu huu akiwa amecheza mechi 24 katika mashindano yote.

No comments:

Post a Comment