Thursday, January 15, 2015

PAMBANO LA PACQUIAO NA MAYWEATHER LAIVA.

PAMBANO lililokuwa likisubiriwa kwa muda mrefu kati ya bondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao linaonekana kukaribia kufanyika. Meneja wa Pacquiao, Fred Sternburg amekanusha ripoti kuwa bondia huyo wa Filipino amekubali tayari kwa pambano la Mei 2 mwaka huu jijini Las Vegas, Marekani. Lakini hata hivyo wakala huyo amesema bado kuna safari ndefu kuelekea katika pambano hilo ili muelekeo sio mbaya sana. Pacquiao mwenye umri wa miaka 36 na Mayweather mwenye umri wa miaka 37 wanahesabiwa kama mabondia bora katika kizazi hiki lakini hawajawahi kupigana. Pacquiao ni bingwa anayeshikilia mkanda dunia wa WBO, wakati Mayweather yeye ni bingwa wa mikanda ya WBC na WBA.

No comments:

Post a Comment