Thursday, January 15, 2015

RONALDO DE LIMA KUREJEA UWANJANI.

NGULI wa soka wa Brazil, Ronaldo de Lima anaweza kurejea tena katika ulimwengu wa soka akiwa na Fort Lauderdale Strikers, ikiwa imepita miaka minne toka atundike daruga. Ronaldo alitambulishwa kama mjumbe mpya wa kundi la wamiliki wa Strikers jana huku kukiwa na ripoti kutoka Brazil zikidai, nguli huyo amenunua asilimia 10 ya hisa za klabu hiyo ya daraja la pili ya Marekani. Akihojiwa mara baada ya kutambulishwa Ronaldo mwenye umri wa miaka 38 amebainisha kuwa anataka kuanza mazoezi ya kujiweka fiti na ana matumaini anaweza kupewa nafasi ya kuvaa jezi ya Strikers. Ronaldo amesema anapenda kucheza soka na ili aweze kurejea tena inabidi ajiweke katika hali nzuri hivyo atalichukulia suala hilo kama changamoto.

No comments:

Post a Comment