Wednesday, January 14, 2015

KIPANDE CHA KOMBE LA DUNIA LILILOIBWA MWAKA 1983 CHAPATIKANA.

KIPANDE cha taji la Kombe la Dunia halisi ambalo liliibiwa nchini Brazil mwaka 1983 na kutowahi kupatikana, kimepatikana katika chumba cha chini katika makao makuu ya Shirikisho la Soka Duniani-FIFA yaliyopo jijini Zurich, Switzerland. Taji hilo ambalo zamani lilikuwa likiitwa Jules Rimet, lilipatikaan sehemu ya chini ambayo bado ilikuwa na majina ya mabingwa wanne wa kwanza wa Kombe la Dunia ambao ni Uruguay walionyakuwa taji hilo mwaka 1930 na 1950 na Italia mwaka 1934 na 1938. Taji ambalo walipewa Brazil moja kwa moja baada ya kushinda Kombe la Dunia kwa mara tatu mwaka 1970 pia liliibiwa miezi mitatu kabla ya michuano hiyo mwaka 1966 iliyofanyika nchini Uingereza. Katika kipindi hicho taji hilo lilipatikana wiki moja baadae baada ya kukutwa kusini mwa jiji la London na mbwa. Rimet ndiye anajulikana kama baba wa Kombe la Dunia kwani alikuwa rais wa FIFA kuanzia mwaka 1921 mpaka 1954. Kipande hicho cha sentimita 10 kinatarajiwa kuwekwa katika makumbusho ya FIFA.

No comments:

Post a Comment