KATIKA tetesi za usajili klabu ya Manchester United inafikiria kutenga kitita cha paundi milioni 25 kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin mwenye umri wa miaka 25 ili kuongeza nguvu katika kikosi hicho. Mbali na mchezaji huyo United pia inamfukuzia mshambuliaji wa Bayern Munich Thomas Muller mwenye umri wa miaka 25 ambaye anataka kuondoka katika timu hiyo. Kwingineko klabu ya Swansea City inamtaka mshambuliaji wa Newcastle United Msenegal Papiss Cisse mwenye umri wa miaka 29 ili kuziba nafasi ya Wilfried Bony anayekwenda Manchester City. Liverpool nao wako tayari kumuuza kiungo Mbrazil Lucas Leiva mwenye umri wa miaka 28 kwenda Napoli kama watafanikiwa kumsajili mshambuliaji nyota wa Aston Villa Fabian Delph. Mabingwa wa Italia Juventus wameonyesha nia ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli mwenye umri wa miaka 24 kwa mkopo mwezi huu huku kukiwa na uwezekano wa kumchukua moja kwa moja katika majira ya kiangazi. Arsenal wanajiandaa kuongeza ofa kwa ajili ya kumnyakuwa kiungo kinda wa klabu ya Legia Warsaw Krystian Bielik mwenye umri wa miaka 17 lakini wanakabiliwa na upinzani kutoka klabu ya Humburg ya Ujerumani. Mshambuliaji nyota wa Tottenham Hotspurs Emmanuel Adebayor yuko katika mazungumzo na Parma lakini kuna uwezekano klabu hiyi ya Italia ikashindwa kutokana na mshahara atakaohitaji.

No comments:
Post a Comment