Tuesday, January 13, 2015

POGBA HAUZWI - JUVENTUS.

MKURUGENZI mkuu wa klabu ya Juventus, Giuseppe Marotta amedai kuwa kiungo Paul Pogba hatauzwa pamoja na vilabu kadhaa barani Ulaya kuonyesha nia ya kumtaka. Klabu ya Manchester United imeripotiwa kujiandaa kutoa ofa ya paundi milioni 77 kwa ajili ya kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 21. Marotta amesema kila klabu Ulaya inamfuatilia nyota huyo na kufanya naye mazungumzo lakini hata hivyo kwasasa wanahitaji kuwa na kikosi imara na Pogba ni sehemu ya kikosi hicho. Pogba amekuwa sehemu muhimu ya kikosi cha Juventus kilichonyakuwa taji la tatu mfululizo la Serie A msimu uliopita akifunga mabao saba na kusaidia mengine zaidi ya saba katika mechi 36 alizoichezea timu hiyo. Nyota huyo ambaye alijiunga na Juventus akitokea United kwa uhamisho huru maka 2012 huku hivi karibuni akisaini mkataba mpya wa kumuweka Turin mpaka mwaka 2019 pia ameripotiwa kutakiwa na timu za Chelsea na Manchester City.

No comments:

Post a Comment