KIUNGO wa klabu ya Real Madrid, Toni Kroos anafikiri Manuel Neuer alistahili zaidi kushika nafasi ya pili nyuma ya Cristiano Ronaldo katika kura za Ballon d’Or kuliko mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina alipata asilimia 15.76 ya kura zilizopigwa akifuatiwa kwa karibu na golikipa huyo wa kimataifa wa Ujerumani aliyepata asilimia 15.72. Hata hivyo Kroos amesema ameshangazwa na kidogo haikuwa halali kwa Neuer kumaliza nyuma ya Messi kwani alistahili kuwa juu yake. Kwa mawazo alidhani ushindani katika tuzo hizo ungekuwa wa karibu zaidi kati ya Neuer na Ronaldo lakini hali ilikuwa tofauti.

No comments:
Post a Comment