MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona Lionel Messi amezua tena mijadala kuhusiana na mustakabali wake baada ya kukiri kuwa hajui atakapokuwa mwaka ujao ingawa amesema anahitaji kubakia katika klabu hiyo ya Catalan. Messi ambaye ni nahodha wa Argentina mwishoni mwa wiki alipuuza tetesi zinazomhusisha kuondoka akidai kuwa sio za kweli. Lakini jana katika sherehe za utoaji tuzo ya Ballon d’Or nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 ameema hakuna mtu anayejua mustakabali wake wa baadae ulipo. Akiulizwa kama anatarajia kumalizia soka lake Barcelona klabu pekee aliyoitumikia mpaka saa au timu ya mji wa nyumbano kwao Rosario, Argentina ya Newell Old Boys, Messi alisitiza na kudai kuwa hajui wapi atakapokwenda kwasasa. Messi amesema siku zote amekuwa akitaka kuendelea kubakia Barcelona lakini katika soka lolote linaweza kutokea hivyo hajui mustakabali wake mwakani utakuwa wapi.

No comments:
Post a Comment