MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amepania kushinda tuzo nyingine ya Ballon d’Or ili kufikia rekodi iliyowekwa na Lionel Messi. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno jana alifanikiwa kuwashinda Messi na golikipa wa Bayern Munich Manuel Neuer katika tuzo hiyo kwenye sherehe zilizofanyika jijini Zurich. Hata hivyo, anaonekana bado hajaridhishwa na tuzo tatu alizopata mpaka sasa na amepania kuongeza nyingine ili kumfikia Messi ambaye amewahi kushinda tuzo hizo mara nne. Akihojiwa Ronaldo amesema tukio hilo ni la kipekee lakini hataki kuishia hapo kwnai anataka kumfikia Messi. Tuzo aliyonyakuwa jana sasa inamfanya Ronaldo kuwafikia nguli wengine wa zamani ambao wamewahi kunyakuwa tuzo hiyo mara tatu akiwemo Johan Cruyff, Michel Platini na Marco van Basten huku Messi pekee ndiye akiwa amenyakuwa tuzo zaidi ya wote hao.

No comments:
Post a Comment