Tuesday, January 13, 2015

STERLING KUONGEZA MKATABA MPYA LIVERPOOL.

MSHAMBULIAJI nyota wa Liverpool Raheem Sterling amekubali kusaini mkataba mpya baada ya kuhakikishiwa mustakabali wake na kocha wa timu hiyo Brendan Rodgers. Sterling amekuwa katika mazungumzo na maofisa wa Liverpool kuhusiana na mkataba mpya kwa miezi kadhaa kufuatia madai kuwa nyota huyo alikataa kuongeza mkataba huku Real Madrid wakiwa tayari kumchukua. Lakini sasa suala hilo linaonekana kwisha kwani nyota huyo wa kimataifa wa Uingereza yuko tayari kuendelea kubakia Anfield. Kikubwa kinachodaiwa kumkwamisha Sterling kusaini mkataba mpya ni kutoelewa mustakabali wa Rodgers ambaye amekuwa naye karibu sana kwani amekuwa akimpa nafasi na kumfanya kung’aa.

No comments:

Post a Comment