WAKALA maarufu Jorge Mendes amesema Cristiano Ronaldo ni mfano wa kuigwa kwa vijana wanaochipukia ambao wanataka kufuata nyayo za mshambuliaji huyo na kudai pia ni mfano kwa watu wazima na jamii ya watu wa Ureno kwa ujumla. Mendes alishuhudia mteja wake akipewa tuzo yake ya tatu ya Ballon d’Or jijini Zurich jana akiwashinda nyota wa Barcelona Lionel Messi na mshindi wa Kombe la Dunia Mjerumani Manuel Neuer. Akizungumza mara baada ya sherehe hizo Mendes amesema Ronaldo ni mchezaji mkubwa na mwenye nidhamu kuwa na anachokifanya ndio maana anaweza kumuita profesa. Wakala huyo aliongeza kuwa bidii zake na mafanikio aliyopata ni mfano tosha kwa viojana wanaochipukia na hata watu wazima.

No comments:
Post a Comment