MSHINDI wa tuzo ya Ballon d’Or, Cristiano Ronaldo amebainisha kuwa meneja mkongwe wa zamani wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson alikuwa akimkumbusha mara kwa mara kuwa yeye ni mchezaji bora duniani. Mshambuliaji huyo wa Real Madrid alikuwa akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo jana akidai kuwa anakumbuka muda wake aliokuwa Old Trafford kwa mapenzi makubwa. Ronaldo ambaye ameitumikia United kwa miaka sita, aliwaambia wana habari kuwa anaikumbuka klabu hiyo kwani pale ndipo alipoanzia na anajua mashabiki wa kule wanamuunga mkono. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa Ferguson aliyekuwa kocha wakati ule alikuwa haishi kumkumbusha umuhimu wake akimwambia kuwa yeye ni bora na asijali kuhusu mengine.

No comments:
Post a Comment