Tuesday, January 13, 2015

CRYSTAL PALACE YAMCHUKUA SANOGO KWA MKOPO.

KLABU ya Crystal Palace imefanikiwa kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Yaya Sanogo kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha Alan Pardew toka aondoke Newcastle United na kuchukua mikoba ya kuinoa Palace mwanzoni mwa Januari. Sanogo alikuwa kihusishwa na taarifa za kujiunga na klabu ya Bordeaux ya Ufaransa lakini Arsene Wenger alikuwa hataki kumtoa kwa mkopo nje ya vilabu vya Uingereza. Akihojiwa Pardew amesema Sanogo ni mchezaji mchanga ambaye ana kipaji na amekuwa akimfuatilia maendeleo yake hivyi anadhani atawasaidia katika kampeni zao katika msimu uliobakia.

No comments:

Post a Comment