Saturday, January 10, 2015

PRINCE ALI AJINADI KUWEKA UWAZI AKICHAGULIWA KUONGOZA FIFA.

MGOMBEA urais katika uchaguzi ujao wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Prince Ali bin Al Hussein amejinadi kuwa atakuwa atalifanya shirikisho hilo kuwa la uwazi na uwajibikaji kama atachaguliwa kugombea kumshinda rais wa sasa Sepp Blatter katika Uchaguzi huo. Prince Ali mwenye umri wa miaka 39 alitangaza mipango yake ya kugombania nafasi hiyo mapema wiki hii na kuapa kusafisha jina la shirikisho hilo ambalo hivi sasa limechaguzi kwa tuhuma mbalimbali za ufisadi. Mwana mfalme huyo wa Jordan amesema kama taasisi FIFA imekuwa ikifanya mambo yake kwa siri hivyo anadhani wakati umefika wa kubadilisha suala hilo na kulileta kwa wakati tunaoishi sasa wa ukweli na uwazi. Uchaguzi wa FIFA unatarajiwa kufanyika Mei 29 mwaka huu huko jijini Zurich.

No comments:

Post a Comment