Saturday, January 10, 2015

VAN GAAL AWAGONGANISHA VICHWA VALDES NA DE GEA.

MENEJA wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal amesema amemsajili Victor Valdes akijua vika kuwa golikipa huyo wa zamani wa Barcelona hatafurahishwa kuwa chaguo la pili mbele ya Mhispania mwenzake David De Gea. Valdes mwenye umri wa miaka 32 amesaini mkataba wa miezi 18 kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford. De Gea mwenye umri wa miaka 24 ndiye golikipa chaguo la kwanza wa United huku akishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa timu hiyo msimu uliopita. Akihojiwa Van Gaal amesema hakuna anayefurahishwa kuwa chaguo la pili na Valdes atakuwa na jukumu la kuhakikisha anamshinda De Gea jambo ambalo halitakuwa rahisi kwake. Valdes amekuwa akifanya mazoezi na United kwa muda kabla ya kusajiliwa wakati akijiuguza majeraha ya goti.

No comments:

Post a Comment