 |
| Ronaldo na Irina wakiwa katika hafla ya Ballon d'Or mwaka jana. |
MSHAMBULIAJI nyota wa klabu ya Real Madrid, Cristiano Ronaldo amethibitisha kutengana na mpenzi wake wa siku nyingi mwanamitindo kutoka Urusi Irina Shayk. Ronaldo alithibitisha taarifa hizo kwa maandishi na kudai kuwa wote wawili wanaamini itakuwa ni bora kuchukua hatua kwasasa kabla ya mahusiano yao hayajaenda mbali zaidi.
 |
| Ronaldo na Irina enzi na mapenzi motomoto. |
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa ametoa taarifa hizo ili kumaliza hali ya tetesi kuhusu mahusiano yake na maisha binafsi. Taarifa za kutengana kwao zilianza kuvuma baada ya Ronaldo kwenda katika sherehe za utoaji tuzo za Ballon d’Or akiwa peke yake jambo ambalo lilikuwa sio la kawaida. Ronaldo amekuwa na mahusiano na mwanamitindo huyo kwa kipindi cha miaka mitano.
No comments:
Post a Comment