Tuesday, January 20, 2015

TORONTO FC YAFANIKIWA KUMNASA NYOTA JUVENTUS.

KLABU ya Toronto FC ya Marekani imfanikiwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Italia na klabu ya Juventus Sebastian Giovinco. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 ambaye amecheza mechi za kimataifa 21 akiwa na Italia anatarajiwa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Toronto haswa baada ya kuondoka kwa Jermain Defoe. Giovinco ambaye ameitumikia Juventus mechi 131, msimu huu umekuwa sio mzuri kwake kwani amefanikiwa kucheza mechi 10 pekee. Mchezaji huyo atajiunga na Toronto ambayo msimu wake unaanzia Machi, mara baada ya kumalizika kwa msimu wa Serie A.

No comments:

Post a Comment