NGULI wa soka wa zamani wa Ureno, Luis Figo anaamini mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wa Barcelona hawangeweza kung’aa na kuwa wachezaji bora wakati wa kipindi anacheza soka. Figo anadhani Ronaldo na Messi ndio wachezaji walio bora kabisa kuliko wengine lakini anahoji kama wangeweza kung’aa kama wangecheza soka katika miaka tisini na mwanzoni mwa 2000. Nguli huyo alikaririwa akidai kuwa kama angekuwa kocha hakuna shaka kwamba angetaka kuwasajili Messi au Ronaldo kwasababu ndio wachezaji bora kwasasa. Hata hivyo Figo aliendelea kudai kuwa enzi zake alipata bahati ya kucheza na wachezaji wazuri na bora katika timu yake na timu pinzani ambao walikuwa bora zaidi ya Ronaldo na Messi hivyo hadhani kama wangeweza kutamba enzi zake.

No comments:
Post a Comment