KATIKA habari za tetesi za usajili zilizopamba vichwa vya habari vya magazeti na mitandao mbalimbali barani Ulaya ni pamoja na meneja wa klabu ya West Bromwich Albion Tony Pulis amemtengea winga wa Wigan Callum McManaman mwenye umri wa miaka 23 kitita cha paundi milioni nne. Mbali na kuwindwa na West Brom winga pia anaripotiwa kuivutia klabu ya Bournemouth huku klabu hiyo ikiwa tayari kumuuza kwa paundi milioni sita. Nao Swansea City wametenga kitita cha paundi milioni nne kwa ajili ya kumsajili beki Martin Olsson wa Norwich huku klabu hiyo ikikubali kumuachia nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 kurejea Ligi Kuu. Klabu ya Manchester United bado wana matumaini ya kumsajili winga wa Real Madrid Gareth Bale mwenye umri wa miaka 25 kwa kitita cha paundi milioni 40 pamoja na kumtoa kipa wake David de Gea ambaye wanamthaminisha kwa paundi milioni 40. Meneja wa Everton Roberto Martinez amesema klabu hiyo imeonyesha kuwa inaweza kufikia matakwa ya winga Kevin Mirallas kabla ya nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji hajasaini mkataba mpya. Kwa upande wa Liverpool wao wametupilia mbali dili la kumrejesha mapema mshambuliaji Divock Origi Anfield. Liverpool walilipa kiasi cha paundi milioni 10 kwa ajili ya kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji katika majira ya kiangazi kabla ya kuamua kumpeleka kwa mkopo katika klabu ya Lille ya Ufaransa. Sasa Liverpool wameamua kuhamishia nguvu zao katika kutaka kumsajili kiungo wa klabu ya Ipswich Town Teddy Bishop mwenye umri wa miaka 18 ambaye ameanza kucheza katika kikosi cha kwanza msimu huu. Beki wa kati wa klabu ya Villarreal Gabriel Paulista mwenye umri wa miaka 24 amekaririwa akidai kuwa wakala wake yuko katika mazungumzo na klabu ya Arsenal juu uwezekano wa kumsajili katika kipindi cha usajili wa Januari.

No comments:
Post a Comment