Monday, January 19, 2015

SASA NIKO FITI - FALCAO.

MSHAMBULIAJI nyota wa Manchester United Radamel Falcao amesisitiza hana majeraha yanayomsumbua na anataka kujihakikishia nafasi ya kuanza katika kikosi cha Louis van Gaal. Baada ya kushindwa kupangwa katika kikosi cha United kilichochapwa bao 1-0 na Southampton Januari 11, nyota huyo wa kimataifa wa Colombia aliitwa tena katika kikosi cha kwanza katika mchezo dhidi ya QPR walioshinda kwa mabao 2-0 ingawa hata hivyo alishindwa kufunga. Baada ya mchezo huo wa mwishoni mwa wiki iliyopita uliofanyika Loftus Road, Van Gaal amekiri kuwa Falcao atafanyiwa tathmini kutokana na mabao aliyofunga lakini mshambuliaji huyo mwenyewe ana uhakika wa kurejesha makali yake ya kufunga kama akipewa nafasi ya kucheza. Falcao amesema dakika 90 ni muhimu kwake kwani anahitaji kucheza na anafurahi kupewa nafasi hivyo ni matumaini yake makali yake ya kufunga yatarejea hivi karibuni. Nyota huyo aliongeza kuwa kwasasa anajisikia vyema kwani anacheza bila kuwa na maumivu yeyote.

No comments:

Post a Comment