MENEJA wa klabu ya Manchester City, Manuel Pellegrini amesema safari ya kikosi chake kwenda kucheza na Chelsea utakuwa ni mchezo muhimu katika kuweka hai matumaini ya kutetea taji lao la Ligi Kuu. City jana walishindwa kupunguza wigo wa alama na vinara Chelsea baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 nyumbani kwao dhidi ya Arsenal, hivyo kuwafanya kuwa nyuma ya vinara hao kwa alama tano. Chelsea wataikaribisha City Januari 31 huku Pellegrini akitambua wazi kuwa ushindi utakuwa muhimu kama wanahitaji kutetea taji lao. Akihojiwa Pellegrini amesema litakuwa jambo muhimu kushinda mchezo wao dhidi ya Chelsea hivyo ni matumaini yao watasahau haraka kipigo walichopata kutoka kwa Arsenal.

No comments:
Post a Comment