Monday, January 19, 2015

TEVEZ BADO MGUU NJE MGUU NDANI JUVENTUS.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina, Carlos Tevez amebainisha kuwa bado hajapata uamuzi wa mwisho kuhusiana na mustakabali wake hivyo anaweza kubakia Juventus. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30 ana mkataba na mabingwa hao wa Serie A ambao unamalizika Juni mwakani lakini hivi karibuni amebainisha kuwa hataki kusaini mkataba mpya hivi sasa na kuzua tetesi kuwa anataka kurejea nchini kwao. Hata hivyo, Tevez amesisitiza kuwa anaweza kuamua kusaini mkataba mpya ili aweze kuendelea kuitumikia Juventus. Akihojiwa na wana habari, Tevez amesema kurudi nyumbani ni wazo alilokuwa nalo na hataki kuwadanganya mashabiki kwani anaweza kubadili wazo hilo wakati wowote.

No comments:

Post a Comment