MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal amesisitiza kuwa hakubadili mfumo wa kiuchezaji katika mchezo dhidi ya Queens park Rangers kutokana na malalamiko ya mashabiki. United ikianza na mfumo wa kuchezesha mabeki watatu nyuma ilishindwa kuonyesha makeke mpaka walipobadilisha na kuanza kucheza 4-4-2 baada ya mashabiki kupaza sauti zao kutoka jukwaani ndipo matunda yalipoanza kuonekana. Lakini Van Gaal amesema kubadili mfumo ilikuwa mipango yake ya kiufundi katika mchezo huo hivyo kwamba amesikiliza mashabiki walichokisema sio kweli. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa United ina mashabiki zaidi ya milioni 600 hivyo hadhani kama ataweza kuchukua maoni ya kila mshabiki. Van Gaal amesema kazi yake ni kuangalia, kuwasiliana, kuchambua na kuona makosa yanayofanywa na wachezaji wake wakiwa uwanjani na sio kusikiliza mashabiki wanasemaje.

No comments:
Post a Comment