MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema ushindi waliopata dhidi ya Manchester City unatoa majibu kuhusiana na watu waliohoji kuhusu safu yao ya ulinzi na uwezo wao wa kuzifunga timu kubwa ugenini. Mabao yaliyofungwa na Santi Cazorla na Olivier Giroud yaliipa ushindi wa mabao 2-0 Arsenal dhidi ya City hivyo kulipa kisasi cha kufungwa mabao 6-3 katika uwanja huohuo wa Etihad msimu uliopita. Akihojiwa Wenger mwenye umri wa miaka 65 amesema amefurahishwa kwasababu safu yao ya ulinzi imekuwa ikikosolewa sana. Wenger amesema malengo yalikuwa kuweka mambo sawa na kushinda mechi kubwa ugenini jambo ambalo walikuwa hawajalifanya msimu huu. Ushindi wa jana unaipaisha Arsenal mpaka nafasi ya tano katika msimamo wa ligi wakiwa kwa alama moja kufikia nafasi ya nne ambayo itawafanya wafuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

No comments:
Post a Comment