Monday, January 19, 2015

AFCON 2015: GYAN HATIHATI KUIVAA SENEGAL.

NAHODHA wa kikosi cha timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan anatarajiwa kuukosa mchezo wa ufunguzi wa timu yake wakati itakapopambana na Senegal baadae hii leo. Timu hizo zitaanza kukwaana huko Mongomo na baadae usiku kufuatiwa na mchezo mwingine kati ya Algeria na Afrika Kusini mechi zikiwa za kundi C. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Ghana ilidai kuwa mshambuliaji huyo alikuwa amepumzishwa katika hospitali iliyopo katika mji wa Mongomo toka Jumamosi jioni na kuruhusiwa Jana asubuhi. Inahisiwa kuwa Gyan alikuwa akisumbuliwa na malaria na tayari amepata matibabu ya awali huku hali yake ikizidi kuimarika.

No comments:

Post a Comment