KATIKA taarifa za tetesi za usajili zilizopamba vichwa vya habari vya magazeti na mitandao mbalimbali barani Ulaya ni pamoja na klabu ya AS Roma imeungana na mahasimu wake wa Italia Inter Milan na Napoli pamoja na klabu ya Besiktas ya Uturuki kwa ajili ya kumuwania winga wa Chelsea Mihamed Salah mwenye umri wa miaka 22. Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema hategemei kufanya usajili mkubwa katika kipindi hiki cha usajili wa dirisha dogo. Naye mshambuliaji wa Everton Samuel Eto’o mwenye umri wa miaka 33 amekubali dili la kurudi tena Italia kwa kusajiliwa na klabu ya Samdoria huku kukiwa na makubaliano ya kuw akocha pindi atakapomaliza mkataba wake wa miaka miwili. Fabian Delph amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia Liverpool lakini meneja wa Aston Villa Paul Lambert amesema bado wana matumaini ya kumshawishi kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25 kusaini mkataba. Klabu za Arsenal na Everton zinamfuatilia kwa karibu winga wa klabu ya Almeira Edgar mwenye umri wa miaka 23 ambapo imeripotiwa kuwa timu hiyo ya Hispania iko tayari kumuuza kwa paundi milioni mbili. Nao Aston Villa wanafikiria kumsajili beki wa klabu ya Lazio Michael Ciani mwenye umri wa miaka 30.

No comments:
Post a Comment