Saturday, January 17, 2015

MSHINDI WA AFCON KUKUNJA DOLA MILIONI 1.5.

SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF katika jarida maalumu kwa ajili ya michuano ya Mataifa ya Afrika-Afcon limeripoti zawadi mbali watakazopata washindi katika michuano hiyo. Timu 16 zinazoshiriki michuano hiyo huko Guinea ya Ikweta zinatarajiwa kugawana jumla ya dola milioni 10. Mshindi atakayenyakuwa kombe hilo atakunja kitita cha dola milioni 1.5 huku anayemfuatia akijipatia kiasi cha dola milioni moja wakati timu zingine mbili ambazo zimeingia nusu fainali zitagawana dola 750,000 kila moja. Timu nane zitakazotinga hatua ya robo fainali zenyewe zina uhakika wa kukunja kitita cha dola 600,000, wakati timu zote zitakazoshika nafasi ya tatu katika makundi yao wtapewa dola 500,000 kila moja. Timu zitakazoburuza mkia katika makundi yao nazo hazitatupwa kwani zitaondoka na kifuta jasho cha dola 400,000.

No comments:

Post a Comment