SHABIKI mmoja amekamatwa baada ya kumvaa meneja wa Arsenal Arsene Wenger wakati wa mchezo wa Ligi Kuu mbao wlaifungwa na Southampton kwa mabao 2-0 jana. Shabiki huyo mwenye umri wa miaka 25 alikuwa akienda kumvaa Wenger mwenye umri wa miaka 65 lakini alizuiwa na mabaunsa kabla ya polisi wa Hampshire hawajamata. Taarifa ya klabu ya Southampton imedai kuwa shabiki huyo alikuwa mshabiki wa Arsenal ambaye alikuwa amekaa jukwaa la mashhabiki wa nyumbani lakini Wenger anadhani alikuwa mshabiki wa Saints. Tukio hilo linakuja baada ya Wenger kushambuliwa na mashabiki wa Arsenal wakati akipanda treni baada ya kipigo dhidi ya Stoke Desemba mwaka jana. Akihojiwa baada ya tukio hilo Wenger amesema anadhani shabiki huyo hakuwa na nia ya kumdhuru kwani hakumsikia hata akisema lolote.

No comments:
Post a Comment